RONALDO AWEKA REKODI APIGA GOLI TANO MADRID YASHINDA 6-0

WANASOKA bora wa dunia, Cristiano Ronaldo amefunga mabao matano peke yake, Real Madird ikiibuka na ushindi wa 6-0 ugenini dhidi ya Espanyol katika La Liga usiku huu Uwanja wa Cornella-El Prat.
Mreno huyo alifunga mabao yake katika dakika za saba, 17 kwa penalti, 20, 61 na 80 wakati bao lingine la Real likifungwa na Karim Benzema dakika ya 28.
Ronaldo sasa anafikisha jumla ya mabao 230 katika mechi 204 za La Liga alizocheza tangu ametua Real, akivunja rekodi ya gwiji wa zamani wa klabu hiyo, Raul aliyefunga mabao 228 katika mechi 550. 
Kikosi cha Espanyol kilikuwa; Lopez, Arbilla, Alvaro, Ciani/Paco Montanes dk46, Duarte, Victor/Joan Jordan dk64, Javi Lopez/Canas dk46, Alvarez, Salva, Gerard na Caicedo.
Real Madrid; Navas, Carvajal, Pepe, Ramos/Varane dk74, Marcelo, Casemiro, Modric/Kovacic dk55, Isco, Bale, Ronaldo na Benzema/Vazquez dk62.
Ronaldo akishangilia baada ya kuweka rekodi mpya ya mabao La Liga, kufuatia kufunga mabao matano peke yake Uwanja wa Cornella-El Pra

No comments

COMMENT

All rights are recieved.. Powered by Blogger.