ARSENAL YAPATA USHINDI WA KWANZA UWANJA WA NYUMBANI
WASHIKA Bunduki wa London wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Stoke City Uwanja wa Emirates, London.
Theo Walcott aliifungia Arsenal bao la kwanza dakika ya 30 kabla ya Olivier Giroud aliyetokea benchi kufunga bao la pili zikiwa zimebaki dakika tano.
Kikosi cha Arsenal kilikuwa; Cech, Bellerin, Koscielny, Gabriel, Monreal, Coquelin, Cazorla, Ramsey, Ozil/Oxlade-Chamberlain dk83, Sanchez/Arteta dk83 na Walcott/Giroud dk75.
Stoke; Butland, Bardsley, Cameron, Muniesa, Pieters, Van Ginkel, Whelan, Shaqiri, Arnautovic, Joselu/Ireland dk57 na Diouf/Bojan dk75.
No comments
COMMENT