MAMILIONNI YA WATOTO WA ATHIRIWA NA VITA
Umoja wa Mataifa umesema kuwa mizozo inayoendelea katika eneo la Mashariki ya Kati, umesababisha zaidi ya watoto milioni 13 kukosa elimu.
Ripoti iliyotolewa na shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, Unicef, matumaini ya vizazi katika eneo hilo la Mashariki ya Kati na Kaskazini mwa Afrika, yameharibiwa.
Ripoti hiyo inasema kuwa zaidi ya shule 9,000 nchini Syria, Iraq, Yemen na Libya zimefungwa.
Shirika hilo la Unicef, pia limenakili mashambulio kadhaa dhidi ya shule na waalim katika maeneo hayo.
Mkurugenzi wa Unicef, katika kanda hiyo Peter Salama, amesema watoto ndio wameadhirika zaidi kwenye mzozo huo.
Amesema licha ya watoto kunyimwa fursa ya kwenda shuleni, wengi wao wamedhulumiwa kimawazo.
Watoto walazimishwa kufanya kazi
Takriban watoto milioni 13.7 ambao hawaendi shuleni, sawa na asilimia 40 ya watoto wanaostahili kuwa shuleni katika mataifa ya Syria, Iraq, Yemen, Libya na Sudan na Umoja wa Mataifa unahofia kuwa idadi hiyo inaweza kuongezeka hadi asilimia 50 katika kipindi cha miezi michache ijayo.
Unicef, imesema kulikuwa na mashambulio 214 yaliyolenga shule mwaka wa 2014 katika mataifa ya Syria, Iraq, Maeneo yanayothibitiwia na Palestina, Sudan na Yemen.
Moja katika ya shule nne imefungwa nchini Syria tangu mwaka wa 2011, na hivyo kuadhiri zaidi ya watoto milioni mbili.
Ripoti hiyo imesema kuuawa, kutekwa nyara na kukamatwa kiholela kwa wanafunzi, waalimu na maafisa wa idara ya elimu katika eneo hilo kumekuwa jambo la kawaida.
Maelfu ya waalimu wamehama kutoka shule zao kutokana na hofu na watoto mara nyingi hulazimishwa kufanya kinyume cha sheria ili kuwasaidia wazazi wao.
Aidha Umoja wa Mataifa, umeonya kuwa kuna hatari ya watoto hao kujiunga na makundi ya waasi wakiwa wachanga.
Salama amesema shirika hilo linahitaji dola milioni 300 zaidi mwaka huu kuimarisha viwango vya elimu katika eneo hilo.AS
No comments
COMMENT