DJOKOVIC:LAZIMA NIJISHINDIE MASHABIKI

Novak DjokovicImage copyrightGetty
Image captionDjokovic amesema anajua hawezi kukaa tu na kukosoa mashabiki
Mchezaji nambari moja duniani katika tenisi Novak Djokovic amesema lazima ajishindie uungwaji mkono wa mashabiki baada yake kuzomewa kwenye fainali ya US Open.
Mserbia huyo aliibuka mshindi kwa kumlaza Roger Federer kwa seti 6-4 5-7 6-4 6-4 uwanjani Flushing Meadows mjini New York Jumapili na kutwaa taji lake la 10 la Grand Slam.
Lakini alipokuwa akielekea kushinda taji hilo lake la kwanza kubwa tangu 2015, alizomewa na mashabiki wa Federer.
“Niko hapa kujishindia uungwaji mkono na natumai siku zijazo nitakuwa hapo,” Djokovic alisema.
Mwanatenisi huyo mwenye umri wa miaka 28 amefanikiwa sana mwaka huu katika Grand Slam, ushindi wake ukijiri baada ya kutwaa mataji ya Australian Open na Wimbledon. Aidha, alifika fainali French Open.
Alishinda mataji matatu ya Grand Slam 2011, lakini alifika nusufainali Paris mwaka huo.
Djokovic alikiri upinzani aliokumbana nao kutoka kwa mashabiki New York ulimtatiza kwa saa tatu na dakika 20 walizocheza lakini “kila mtu hupanda na kushuka katika umakinifu”.
“Muhimu ni kukumbuka mambo ya kimsingi na kujua ni kwa nini uko hapo na wahitaji kufanya nini.”
"Kila mtu ana uhuru wa kumuunga mkono mchezaji anayetaka.”

No comments

COMMENT

All rights are recieved.. Powered by Blogger.