DAKTARI WA CHELSEA EVA AAMUA KUMKACHA MOURIHO

2B54DAC400000578-3196584-Mourinho_looks_on_as_Chelsea_managed_to_hang_on_and_draw_2_2_wit-m-11_1439474541465Presha imezidi kuwa kubwa kwa kocha Jose Mourinho wa Chelsea mara baada ya daktari Eva Carneiro kutoweka klabuni na sasa anawasiliana na wanasheria wakubwa kumsaidia kudai haki zake.
Eva na Mourinho waliingia katika mzozo siku ya tarehe 8 mwezi uliopita katika mchezo wa sare ya bao 2-2 dhidi ya Swansea, baada ya Mourinho kumshutumu Eva kuwa sababu ya wao kutopata ushindi katika mechi hiyo kwa kuwa alienda uwanjani kumtibia Eden Hazard.
Baada ya Mourinho kumuadhibu mwanadada huyo kwa kumkataza kukaa katika benchi la Chelsea, lakini pia kutofika hotelini, mwadada huyo mwenye asili ya Gibraltar aliondoka klabuni hapo na sasa amegoma kurudi tena kikosini kwa madai yakutoweza tena kufanya kazi na Mourinho.
Imeelezwa kuwa kocha Jose Mourinho alitoa kauli za matusi na ubaguzi baada ya kumtamkia dada huyo maneno ya lugha chafu akizungumza kwa kireno na sasa dada huyo baada ya kutopata sapoti ya klabu, ameamua kuikacha klabu hiyo na kutafuta haki mahali kutako stahiki.
Mourinho anaweza kuwa matatani baada ya FA kupata ushahidi wa kauli hizo za kibaguzi za Mourinho huku pia chama cha madaktari nchini England kikitaka FA ichukue hatua.

No comments

COMMENT

All rights are recieved.. Powered by Blogger.