AUNT EZEKIEL;NIMEAMUA KURUDI CMM NA SIJAPEWA HELA WALA GARI
MWIGIZAJI mahiri wa filamu nchini, Aunt Ezekiel, amedai kutishiwa amani baada ya kufanya maamuzi yake kisiasa ambapo amehamisha ushabiki wake kutoka CHADEMA na kwenda CCM.
Licha ya mrembo huyo kudai kupokea vitisho mbalimbali, pia alidai amehama chama hicho na kujiunga na CCM kutokana na kukubali sera za chama hicho.
“Sera za chama nilichohamia zimenivutia na wala sikulazimishwa na mtu wala sijapokea fedha wala gari kuhamia huko kama inavyosemekana, bali nafsi na mapenzi pamoja na haki yangu ndiyo yaliyonipeleka huko.
“Nashangaa maamuzi yawe yangu bado watu wanitumie jumbe za vitisho, mimi ni raia kama walivyo wengine, umaarufu wangu usiwe sababu,” alisema Aunt, ambaye awali alikuwa akivaa magwanda CHADEMA

No comments
COMMENT