ANGELA MERKEL AZUMNGUMZIA MZOZO WA SYRIA
Ujerumani imesema Rais wa Syria Bashar al-Assad, anapaswa kushiriki katika mazungumzo yenye lengo la kumaliza mzozo wa nchi yake uliodumu kwa zaidi ya miaka minne sasa.
Kansela Angela Merkel amefafanua kuwa mchakato wa mazungumzo hayo unapaswa pia kuihusisha Marekani na Urusi na nchi za ukanda huo, zilizo muhimu katika utatuzi wa mgogoro huo ambazo ni Iran na Saudi Arabia.
Wiki iliyopita, Marekani ilikataa wito uliotolewa na Rais wa Urusi Vladmir Putin, kushirikiana na serikali ya Rais Assad kuweza kuwashinda wanamgambo wa Kiislamu walioko Syria na Iraq.
No comments
COMMENT