SAIDA KAROLI ATISHIWA KUUAWA

Msanii wa muziki wa asili nchini Tanzania, Saida Karoli amedai amepokea taarifa kwamba kuna watu wanataka kumuua.
Said Karoli ambaye sasa anafanya vyema na wimbo wake ‘Orugambo’ amedai amesitisha baadhi ya show zake kutokana na sakata hilo ambalo amedai inaratibiwa na wapinzani wake ambao wanataka kumpoteza kwenye muziki.
“Huyo mtu alinielekeza watu kadhaa ambao wamepanga mpango wa kuniua aliniambia, sasa mimi nimeshalipwa nikuuwe nikuondoe duniani kabisa yaani kabla ya kufika Mwanza, Geita tena bora hata hizi show zingine uvunje, kweli ramani aliyonipa nilichoka ikabidi show zingine za Bukoba tumezivunja tukasema ngoja tutulie kwanza tuone nini kitaendelea” alisema Said Karoli 
Saida Karoli anakiri wazi kuwa suala la ushirikiana lipo na kwake si jambo la ajabu kumtokea kwani tayari ameshakutana na mambo ya namna hiyo sana na kudai yeye anamtegemea Mungu na kumuomba Mungu

No comments

COMMENT

All rights are recieved.. Powered by Blogger.