"NYUMBA NIJENGE KWA SHIDA LEO NIBOMOLEWE BILA FIDIA"? -Profesa Jay
Moja ya story inayosambaa kwenye mitandao ni pamoja na hii inayomhusu Mbunge wa Mikumi Joseph Haule ‘Profesa Jay’ ambaye nyumba yake iliyopo Mbezi kuwekwa alama ya X ikiwa ni miongoni mwa nyumba zitakazobomolewa ili kupisha upanuzi barabara.
Profesa Jay amezungumza kwenye 255 ya XXL ya Clouds FM leo August 4, 2017 na kuthibitisha kuwekewa alama ya X kwenye nyumba zao zikitakiwa kuvunjwa kutokana na kujenga ndani ya hifadhi ya barabara huku wakiungana kwenda kuiomba Mahakama iwapatie haki.
>>>“Ni kweli ni mewekewa X hapa tunatakiwa tuvunje kama ilivyokuwa kwa wengine. Tumeungana na majirani na watu wengine ikiwemo Serikali ya Mtaa, Mbunge wetu na Diwani kwenda kufungua kesi kuomba huu upana wanaosema kwamba wa barabara kupanua Mita 121.5 upo kinyume na utaratibu ambao na sisi tunaufahamu. Ni sehemu kubwa sana na watu wemgi wataathirika. Tunaamini kwamba haki inapatikana.
“Kitu ambacho tumekuwa tukikisisitiza hakuna mtu anayekataa kuhama kwa ajili ya maendeleo lakini unapomwambia mtu abomolewe nyumba yake kwa hiyo sheria iliyobadilishwa 2007 lakini ni sheria ya mwaka 1932. Hivyo kwa sheria kama hizo ni sheria kandamizi. Hii nyumba nimejenga muda refu sana kupitia muziki. Unapewa Laki Mbili unanunua misumari nyingine unakula bata. Si unajua enzi za ujana tulivyokuwa tunafanya.
“Kwa hiyo, tumejenga kwa taabu na ni miaka mingi sana, sasa unapokuja kuona kuwa inabomolewa siku moja inaangushwa wakati unasikia hakuna fidia, Serikali inabadi iangalie kwa jicho pana na jicho pevu kwa kuangalia kuwasaidia wananchi wengi ambao kiukweli wanaumia sana.” – Profesa Jay
No comments
COMMENT