NDOTO ZA KIMAREKANI ZA DIAMOND KWA ALIKIBA ZIMEDUNDA

Kwa takribani miaka mitatu sasa mafahari wawili wa muziki wa kizazi kipya yaani Bongo Flava Alikiba na Diamond Platinumz wamekuwa katika bifu zito sana, licha ya wao kujaribu kila siku kuukwepa ukweli huo. Hakuna kati yao ambaye amewahi kujitokeza hadharani na kukiri uhasama kati yao lakini ni wazi kuwa watu hawa hawapikiki chungu kimoja.
Mara kwa mara watu wa karibu wa Diamond wakiwemo watu walio kwenye management yake hususan, mameneja Sallam na Ricardo Momo, wamekuwa wakimtupia vijembe Alikiba. “Wao wakipost tembo, sisi tunapost show” na “waambie dada zao Kariakoo waje Ulaya” ni baadhi tu ya mistari ambayo Diamond amewahi kusikika akiimba ikiwa ni kuelekeza mashambulizi upande wa Alikiba na kambi yake.
Hivi karibuni Diamond akiwa kwenye Interview ya kipindi cha 360 cha Clouds FM, alikaririwa akisema kuwa hana tatizo na Alikiba, ni mtu anayeheshimiana naye na hata uongozi wake uko katika mazungumzo na uongozi wa Alikiba ili Kiba aweze kuuza nyimbo zake kwenye mtandao wa wasafidotcom ambao ni mradi mpya wa Diamond.
Baadaye usiku kupitia akaunti yake ya Instagram Alikiba aliandika caption zenye utata zilizotafsiriwa na mashabiki na wadau mbalimbali kuwa zimelenga kujibu maneno hayo ya Diamond Platnumz.
Wamarekani wana sera zao mbili ambazo wanazitumia sana katika kulifanya taifa lao kuendelea kuwa taifa kubwa duniani. Sera ya kwanza; njia pekee ya kumshinda adui ni kumfanya rafiki, ya pili; wamarekani hawahitaji rafiki dhati wala adui kweli, zaidi ni kutimiza interest zao.
Hivyo watakufanya rafiki ili wapate watakacho na utarudi kuwa adui wakishatimiza azma yao. Lakini Waingereza pia wanasema numbers don’t lie. Nimejaribu kufuatilia rekodi za nyuma za Alikiba katika mtandao wa mkito.com nikagundua kuwa Alikiba ni record breaker. Mwana iliweka rekodi, Chekecha Cheketua iliweka rekodi. Hata nyimbo ya Nisamehe aliyoshirikishwa na Barakah Da Prince pamoja na nyimbo ya Kajiandae aliyoshirikishwa na Ommy Dimpoz zimeingia kwenye Top 5 ya ngoma zilizopakuliwa zaidi kwenye mtandao wa Mkito mwaka 2016.
Kwa rekodu hizi ni dhahiri Diamond anahitaji amani na Alikiba kwasababu za kibiashara zaidi. Anatambua fan base aliyonayo Alikiba itabust zaidi mtandao wake, pesa atakayopata ni kubwa, pia number of visitors itaongezeka kwa kasi kwani kila mtu atataka kuamini ni kweli Ali yumo? Haikushangaza kuona editing kwenye mitandao ikionesha kua profile ya Alikiba ipo kwenye wasafidotcom.
Kwa hali ilivyo sioni na sidhani kama management ya Alikiba itaweza kukubali kuuza nyimbo kwenye mtandao wa Diamond. Kwanza wanajiamini sababu wameshauza kabla na kuweza kuweka baadhi ya rekodi kwenye mtandao wa Mkito. Pili kutoka kwa mfululizo wa mashambulizi ya maneno kutoka kwa Dimond na management yake kwenda kwa Alikiba itakuwa ni fedheha kubwa kwa mashabiki wa Ali kama Ali na uongozi wake utakubaliana na suala hili. Na ndio maana nasema sera za kimarekani za Dimond zimedunda kwa Alikiba.

No comments

COMMENT

All rights are recieved.. Powered by Blogger.