Q CHILLAH AFUNGUKA KUHUSU KUSHINDWA KUFANYA VIDEO

Msanii wa Bongo Flava, Q Chillah ameeleza kushindwa kutoa video ya ngoma yake ‘Naogopa’.
Muimbaji huyo ameiambia Dj Show ya Radio One kuwa yeye anahitaji kufanya video itakayomrudisha ambayo ni gharama kubwa kitu ambacho anakishughulikia kwa sasa.
“Nia yangu ilikuwa audio na video kwa pamoja kwa sababu hiki ni kitu ambacho msanii anapaswa kufanya. Tumekwama kwa maana nilitaka kufanya video nzuri na bora, siyo bora tu video na siyo kukurupuka kwa sababu wenzangu wanatoa. Kumrudisha Q Chillah ni lazima tutulie, tutulize akili tujaribu kufanya video ambazo zinateka soko, zinaweza kumsogeza kupata show, kupata mikataba mikubwa,” amesema na kuongeza.
“It need big budget am work in it nikiendelea kuongea na taasisi na kaka zangu, wadau wa muziki lakini pia wawekezaji, kwa hiyo tupo kwenye changamoto hii kwa sasa,” amesisitiza.

No comments

COMMENT

All rights are recieved.. Powered by Blogger.