KIONGOZI WA ZAMANI WA KUNDI LA WAASI "Al Shabaab" AJISALIMISHA
Maafisa nchini Somalia wamesema aliyewahi kuwa kiongozi wa juu wa kundi la al-Shabaab, Mukhtar Robow amejisalimisha kwa majeshi ya Serikali katika mji Huddur magharibi mwa Somalia.
Bwana Robow alikuwa kiongozi na msemaji mkuu wa kundi la al-Shabaab kabla ya kutofautiana na kundi hilo miaka minne iliyopita.
Mwezi Juni mwaka jana 2016, Marekani iliondoa zawadi ya dola milioni tano kwa bwana Robow ambaye bado anaaminiwa kuendelea na shughuli zake kama mwanamgambo.
Al Shabab bado inadhibiti maeneo makubwa ya Somalia na kufanya mashambulizi ya mara kwa mara nchini Somalia na nchi jirani ya Kenya.
No comments
COMMENT