Grace" Matata: Natamani sana kufanya collabo na Nandy"

Msanii wa Bongo Flava, Grace Matata amesema anafurahishwa na wasanii wapya wa kike wanaokuja katika muziki huo na kufanya vizuri.
Miongoni mwa wasanii hao amemtaja Maua Sama ambaye ameshawahi kutoa naye wimbo ‘Hellow’ na Nandy ambaye amebainisha anatamani kufanya naye kazi.
“First of all I love Nandy, I think Nandy is very good singer, I think Maua Sama is amazing singer na nimefanya naye kazi na ningependa kufanya kazi na Nandy and am so happy kuona young women wanakuja in a music industry na wanafanya big thing,” ameiambia EA Radio.
Ameongeza kuwa haumii anapoona wasanii hao wanapokuja na kufanya vizuri kwani kila mtu ana malengo yake kwa kile anachokifanya, “one thing na kila siku nazidi kusisitiza music is not competition, muziki ni mission kila mtu ana mission yake” amesema Grace Matata.
Kwa sasa hitmaker huyo wa ngoma kama Free Soul, Uwe Wangu, Wimbo Wangu, Utanifaa na nyinginezo anafanya vizuri na ngoma mpya ‘Dakika Moja’ ambayo amemshirikisha rapper Wakazi. 
#DbashHeadlinesBlog 

No comments

COMMENT

All rights are recieved.. Powered by Blogger.