FAMILIA ZILIZO POTEZA NGUGU KWENYE SHOW YA ARIANA GRANDE WALIPWA
Takribani miezi mitatu baada ya watu 22 kupoteza maisha kwenye mlipuko wa bomu katika show ya Ariana Grande mjini Manchester, Emergency Fund imesema itawapa $324,000 kila familia iliyopoteza mtu kwenye show hio.
Gazeti la The Guardian limesema tayari familia hizo zimeshapokea $90,000 na watamaliziwa zingine baadae.
Pesa hizi zinatoka kwenye dola milioni 24.5 zilizochangishwa baad aya mlipuko wa bomu kwenye ukumbi wa Manchester Arena, alipofanya show Ariana Grande katika show yake ya “Dangerous Woman World Tour.” na dola milioni 2 zilitoka kwenye show ya “One Love” iliyofanyika June.
No comments
COMMENT