Baada ya mjengo wake kupigwa mnada Profesa Jay afunguka haya.
Msanii wa hip hop Bongo na Mbunge wa jimbo la Mikumi Joseph Haule ‘Professor Jay’, amezungumzia taarifa za nyumba yake iliyopo Kimara Dar es Salaam kupigwa alama X kama ishara ya kutakiwa kuvunja na kuondoka ili kupisha upanuzi wa barabara.
Rapper huyo mkongwe amesema ni kweli yeye na majirani zake wamewekewa X ila wameungana na serikali ya mtaa, kitongoji, mbunge na diwani kuomba mahakamani kwamba upana tajwa ni mkubwa sana na ni kinyume na utaratibu ambao wanaufahamu wao.
“Wanasema kupanua ni meta 121.5 ni upana mkubwa sana na upande mkubwa sana na watu wengi wataarithirika na wataumia. Kwa sababu tunaamini haki inapatikana mahakamani ndio maana tukaenda kuweka zuio, kuangalia ni jinsi gani tunaweza kupata haki yetu ya msingi lakini kitu kikubwa tunachozidi kusisitiza hakuna mtu anayekataa kuhama kwa ajili ya maendeleo,” Professor Jay ameimbia XXL ya Clouds Fm na kuongeza.
“Wengine tumejenga kwa muda mrefu sana, nakumbuka hii nyumba nimejenga kupitia muziki, unapata lakini mbili unatoa elfu hamsini unanunua misumari halafu laki na nusu unakula bata, kwa hiyo unapoona kwamba inabomolewa kwa siku moja na hakuna fidia serikali inatakiwa iangalia kwa jicho pevu,” amesema Professor Jay.
#DbashHeadlines
No comments
COMMENT