UCHUNGUZI WA SNDELEAHAMBULIO MJINI NICE WAE
Mwendesha mashitaka nchini Ufaransa amesema kuna ushahidi kwamba mtu aliyekuwa anaendesha lori na kutekeleza shambulizi katika mji wa Nice wiki iliyopita kwamba siku za hivi karibuni alikuwa na mahaba na makundi yenye harakati za kigaidi na msimamo mkali wa kidini.
Kiongozi mkuu wa uchunguzi wa shambulizi hili, Francois Molins aliangazia mtandaoni mahali ambapo mshambuliaji Mohamed Lahouaiej-Bouhlel ambaye ana asili ya Tunisia alikuwa akisakura.
Ingawa ameeleza kwamba wadadisi wa mambo mpaka sasa baso hawajaweza kuthibitisha kwamba ana nasaba na makundi ya kigaidi.Mwendesha mashitaka amemwelezea mshambuliaji aliyetekeleza shambulizi na kuuawa watu themanini na wanne kama mtu aliyerukwa na akili katika utekelezaji wa vitendo vya kigaidi.
Alitoa mfano wa maelezo ya harakati za Lahaie-Bouhlel sikukadhaa kabla ya shambulio hilo na wakati wa mpango wa kukodisha lori lililohusika katika tukio hilo.
Awali waziri mkuu wa Ufaransa, Manuel Valls alizomewa wakati alipokuwa akijiandaa kujiunga katika maombolezo ya dakika chache za ukimya nchini kote Ufaransa, na Vallas ameita kitendo hicho kama ukosefu wa nidhamu na cha kudhalilisha
No comments
COMMENT