CHID BENZ AKATAA 'ASEMA AKUTOA WIMBO WA MATUSI BALI ULIVUJA
Msanii wa Hip Hop Chid Benz amefunguka na kusema kuwa hakukusudia kutoa freestyle ambayo alisikika yeye akichana na kutukana matusi mengi bali kuna mtu aliivujisha.
Chid alisema hata wakati akiwa anachana freestyle hiyo hakuwa anajua kuwa anarekodiwa na aliyemrekodi hajaonana naye mpaka leo kuwa yuko nje ya nchi.
“Nilikuwa niko booth nafanya freestyle kimpango wangu kumbe jamaa kabonyeza record, baadaye akaitengeneza na kuvujisha kwenye mitandao,ikazagaa mpaka marekani..Mimi nilichukizwa sana,inaonekana nilifanya makusudi.hata kama watu waliipenda mimi binafsi sikuipenda“alifunguka chid kuhusiana na Freestyle hiyo iliyozagaa miaka kadhaa nyuma.
No comments
COMMENT