KOCHA WA TIMU YA TAIFA MKWASA ATANGAZA KIKOSI CHA TAIFA STARS ATAJA MAJINA MAPYA
Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars inajiandaa kucheza hatua ya pili ya michuano ya kuwania kufuzu kucheza Kombe la Dunia 2018 Urusi. Tanzania ambayo itacheza mchezo wake wa kwanza wa hatua ya pili ya kuwania kufuzu michuano hiyo November 14 uwanja wa Taifa Dar Es Salaam dhidi ya Algeria.
Kupitia kwa kocha wa timu hiyo Charles Boniface Mkwasa ametangaza kikosi cha wachezaji 28 watakaoingia kambini November 1 Dar Es Salaam na November 2 kusafiri kuelekea Oman Muscut kwa kambi ya siku 11. Mkwasa ametangaza majina manne mapya kikosini, ambayo ni Elias Maguli, Malimi Busungu, Hassan Kessy, Salim Mbonde na kuwaongeza Jonas Mkude na Salum Abubakar ambao hawakuitwa kikosini kwa siku za hivi karibuni
Majina 28 ya Kikosi cha Taifa Stars kilichotangazwa leo October 27 mbele ya waandishi wa habari
MAGOLIKIPA
- Ally Mustafa Yanga
- Aishi Manula Azam FC
- Saidi Mohamed Mtibwa Sugar
MABEKI WA PEMBENI
- Shomari Kapombe Azam FC
- Mwinyi Haji Yanga
- Mohamed Hussein Simba
- Hassan Kessy Simba
- Juma Abdul Yanga
MABEKI WA KATI
- Nadir Haroub Yanga
- Kelvin Yondani Yanga
- Salim Mbonde Mtibwa
- Hassan Isihaka Simba
VIUNGO
- Himid Mao Azam FC
- Mudathir Yahaya Azam FC
- Jonas Mkude Simba
- Salum Abubakar Azam FC
- Said Ndemla Simba
- Salum Telela Yanga
- Frank Domayo Azam FC
WINGA
- Thomas Ulimwengu TP Mazembe
- Farid Musa Azam FC
- Simon Msuva Yanga
- Mrisho Ngassa Free State
WASHAMBULIAJI WA KATI
- Mbwana Samatta TP Mazembe
- John Bocco Azam FC
- Elias Maguli Stand United
- Malimi Busungu Yanga
- Ibrahim Ajib Simba
No comments
COMMENT