FAINALI YA KLABU BINGWA AFRIKA YAPIGWA LEO JE SAMATA ANAWEZA WEKA REKOD LEO
Michuano ya fainali ya klabu Bingwa Afrika inatarajia kufanyika leo October 31 nchiniAlgeria kwa mchezo wa kwanza wa fainali hiyo kupigwa, huu ni mchezo ambao hisia za watanzania wengi wamezielekeza huko kwa kuwatazama mastaa wa soka waTanzania ambao wanatazamiwa kucheza katika mechi hiyo Samatta na Ulimwengu.
Mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika unachezwa leo October 31 kwa kuzikutanisha timu za US Alger ya Algeria dhidi ya TP Mazembe ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo ambayo inachezewa na watanzania wawili Mbwana Samatta naThomas Ulimwengu, stori ni kuwa Mbwana Samatta huenda akaweka rekodi ya kuwa mfungaji bora wa michuano hiyo kwani hadi sasa ana goli 6 hivyo kama atafanikiwa kufunga katika mechi mbili za fainali anaweza twaa tuzo ya mfungaji bora.
Klabu ya TP Mazembe imewahi kutwaa klabu Bingwa Afrika mara nne wakati wapinzani wao US Alger hawajawahi kutwaa Kombe hilo hata mara moja, hivyo kila timu inaingia uwanjani ikihitaji ushindi, kwa kawaida fainali ya Klabu Bingwa Afrika huchezwa nyumbani na ugenini hivyo baada ya mechi ya October 31 US Alger watasafiri kwenda kucheza fainali ya pili Lubumbashi Kongo November 8.
No comments
COMMENT