ALBUM YA RIHANA IPO NJIANI APATA DILI KUBWA YA KUPROMOT ALBUM YAKE
Rihanna kwenye healines mtu wangu, baada ya kutudokeza cover mpya ya Album yake mpya ‘Anti’ msanii huyo pamoja na management yake imeamua kuingi mkataba na kampuni kubwa ya simu duniani, Samsung kwa ajili ya kusponcer na kupromote ujio wa Album hiyo pamoja na Tour yake.
Kwa mujibu wa mtandao wa New York Post, mkataba wa Rihanna na Samsung utakuwa wa miezi saba baada ya msanii huyo kuamua kufanya mabadiliko kadhaa kwenye Album yake mpya ya ‘Anti’.
Jay Z amabaye ndiye Mkurugenzi wa Roc Nation label aliyopo Rihanna na Jay Brownambaye ndiye Manager wa msanii huyo walisaidiana kukamilisha dili hiyo yenye thamani ya dola Milion 25 sawa na Tzs. Bilion 55 kwa niaba ya Rihanna.
Samsung ina mipango ya kushirikiana na Rihanna kwenye hili sio tu kwa kusponcer na kupromote Album na Tour yake bali pia kupromote simu zao aina ya The Galaxy Brand… lebo ya Rihanna, Roc Nation pia inafahamika kuwa na historia nzuri ya mahusiano na kampuni hiyo ya simu ambayo mwaka 2013 kampuni hiyo kutoka South Korea ilinunua zaidi ya copy milioni moja ya Album ya Jay Z, Magna Carta.
Kwa sasa lebo ya Roc Nation na Rihanna mwenyewe bado wanajadiliana tarehe nzuri ya kuileta sokoni Album mpya ya msanii huyo, Anti
No comments
COMMENT