RAIS WA MAlDIVES ANUSURIKA MLIPUKO
Rais wa Maldives Yameen Abdul Gayoom , amenusurika bila majeraha baada ya mlipuko kutokea kwenye boti yake alipokuwa akirejea nchini humo baada ya kuhiji Saudi Arabia.
Waziri Mohamed Shareef amesema mlipuko huo umetokea boti hiyo ya mwendo wa kasi ilipokuwa ikiingia eneo la kuegesha boti katika mji mkuu Male.
Mkewe rais huyo Fathimath Ibrahim na mmoja wa msaidizi wake wamepata majeraha madogo, amesema. Hata hivyo mlinzi mmoja amepata majeraha mabaya.
Shareef amesema chanzo cha mlipuko huo, unaodaiwa kuanza eneo la injini la boti hiyo, bato hakijabainika.
Ajali za boti hutokea mara kwa mara katika taifa hilo la visiwa linalopatikana katika Bahari ya Hindi.
Uwanja mkuu wa taifa hilo umo kwenye kisiwa tofauti na wasafiri hulazimika kutumia boti kufika kisiwa kilicho na mji mkuu.
Ahmed Hamdhoon, mwanahabari aliyekuwa ameenda kufuatilia kuwasili kwa Gayoom, “Hatujafutilia mbali uwezekano wa mlipuko huo kusababishwa na chochote, inaweza kuwa ajali au jaribio la kumuua rais,” Shareef alisema na kuongeza kuwa wachunguzi wanachunguza boti hiyo na video kuhusu mlipuko huo.
amesema alisikia mlipuko mkubwa muda mfupi baada ya boti kuwasili.
“Mlango wa kulia wa boti uling’oka na kuanguka na kukawa na moshi mwingi. Watu walikuwa wakilia,” alisema.
Kisiwa cha Maldives, kijulikanacho kutokana na hoteli za kifahari za baharini, kimekumbwa na mizozo ya kisiasa na uchaguzi uliokuwa na utata, lakini hakujakuwepo na visa vikubwa vya watu kushambuliwa kwa mabomu.
No comments
COMMENT