RAIS WA GABON AISHUTUMU UFARANSA
Rais wa Gabon Ali Bongo amesema kuwa kukamatwa kwa mkuu wa majeshi wa taifa hilo mjini Paris mnamo mwezi Agosti ni jaribio la kuifedhehesha Gabon.
Bwana Bongo alikuwa akizungumza katika makao rasmi ya rais Francois Hollande baada ya kukutana naye mjini Paris.
Mkuu huyo wa majeshi Maixent Accrombessi alizuiliwa kwa mda katika uwanja wa ndege wa Charles de Gaulle kwa tuhuma za madai ya ufisadi baada ya kandarasi ya sare za kijeshi nchini Gabon kupewa kampuni moja ya Ufaransa kulingana na chombo cha habari cha AFP.
No comments
COMMENT