MAPATO YA MAN U YASHUKA
Mapato ya kilabu ya Manchester United yalianguka kwa pauni milioni 38 msimu uliopita baada ya kushindwa kufuzu katika mechi za vilabu bngwa Ulaya.
Jumla ya mapato ya timu hiyo ni pauni milioni 395.2 chini kutoka pauni milioni 433.2 lakini fedha za ufadhili ziliongezeka na kuvunja rekodi kwa asilimia 14 na kufikia pauni milioni 154.9 .
Hatua hiyo ilisababisha mapato ya watu wanaoingia uwanjani kushuka kwa asilimia 16 na kufikia pauni milioni 90.6 huku mapato ya utangazaji yakishukana kufikia pauni milioni 107.7 ambapo kimeshuka kwa kitita cha pauni milioni 28.1.
Kutofuzu kwa kombe la vilabu bingwa Ulaya kuliigharimu kilabu hiyo pauni milioni 35 kupitia mapato ya mechi na yale ya utangazaji.
No comments
COMMENT