LIGI YA MABINGWA ULAYA YATARAJIWA KUENDELEA KESHO
Michezo ya pili ya michuano ya klabu bingwa itaendelea tena kushika kasi hapo kesho kwa michezo nane kuchezwa.
Katika kundi E Barcelona itakua katika dimba lao la Camp Nou, kuwaalika Bayern Leverkusen kutoka Ujerumani mchezo huku Bate wakiwalika As Roma mchezo utaopigwa katika uwanja wa Borisov-Arena.
Katika kundi F Arsenal ya England itakipiga na Olympiakos ya Ugiriki, wakati miamba wa Ujerumani Bayern Munich wao wakishuka dimbani kuwakabili Dinamo Zagreb ya Croatia.
Michezo mingine itayopigwa hapo kesho ni
Kundi G
FC Porto na Chelsea
Maccabi Tel Aviv na Dynamo Kiev
Kundi H
Lyon v Valencia
Zenit St Petersburg v KAA Gent
No comments
COMMENT