HAKUNA KAMA MIMI "MOURINHO AJIGAMBA
Mkufunzi wa Chelsea Jose Mourinho amesisitiza kuwa yeye ni bora kushinda yeyote yule katika kuifunza kilabu hiyo licha ya mabingwa hao watetezi wa ligi ya Uingereza kushindwa vibaya katika kipindi cha miaka 29.
Aliyekuwa mshambuliaji wa Uingereza Chris Sutton ameonya kuwa Chelsea wanarudi nyuma baada ya kushindwa kwa mara ya tatu msimu huu.
Hii ni mara ya kwanza kwa Mourinho kuwa na shinikizo katika kazi yake akiwa Chelsea.
Kufuatia kichapo hicho cha mabao 3-1 dhidi ya Everton ,Mourinho alisema kuwa watu wengi sasa wanafurahia janga lake.
''Haya ni matokeo mabaya zaidi katika kazi yangu'', alisema Mourinho.
''Sijazoea mambo kama haya lakini sasa nimeanza kuyaelewa katika kazi yangu.Hatahivyo sihisi shinikizo yoyote'',aliongezea.
''Mimi ndiye ninayefaa kwa kazi hii .Sidhani kama kuna mtu zaidi yangu anayeweza kuifanya kazi hii'',alisema.
No comments
COMMENT