USAIN BOLTI BINGWA WA DUNIA

Mwanariadha wa Jamaica Usain Bolt, ameshinda medali yake ya pili ya dhahabu, katika mashindano ya riadha ya dunia yanayoendelea mjini Beijing nchini Uchina.
Bolt alitimuka mbio hizo kwa muda wa sekunde 19.55 na kunyakulia taifa lake medali nyingine mbali na kuandikisha rekodi ya kuwa mwanariadha kasi zaidi duniani katika mbio za masafa mafupi.
Ushindi huo ni wa kumi kwa mwanariadha huyo kutoka Jamaica na ni ya nne mfululizo katika mbio hizo za dunia.
Justin Gatlin wa Marekani, pia alishinda medali ya fedha katika mbio za mita mia moja, alimaliza wa pili akifuatwa na Gatlin alitumia sekunde 19.74.

No comments

COMMENT

All rights are recieved.. Powered by Blogger.