UNHCR YAPATA DOLA MILIONI 6 ZA WAKIMBIZI

Umoja wa mataifa umetangaza msaada wa dola milioni 6 kama msaada wa kibidamu kwa wale wanaokimbia mzozo nchini Yemen na kutafuta hifadhi nchini Djibouti na Somalia.
Msaada huu mpya kwa Yemen mwaka 2015 unafikisha karibu dola milioni 81 zilizotolewa na umoja wa mataifa.
Image captionWakimbizi wa Yemen
Msaada huu ni mchango kwenda Djibouti na Somalia kufuatia ombi kutoka kwa ofisi ya shirika la kuhudumia wakimbizi la umoja wa mataiafa UNHCR.
Msaada huo utaiwezesha UNHCR kuwapa makao wakimbizi walio nchini Somalia na Djibouti, pamoja na maji safi na huduma za afya, pamoja na mipango inayowalinda watoto na huduma zinazozuia unyanyasaji wa kijinsia.

No comments

COMMENT

All rights are recieved.. Powered by Blogger.